UJERUMANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Ujerumani yajiandaa kwa chanjo mwishoni mwa mwaka 2020

Berlin mwezi uliopita ilitenga fedha milioni 745 kwa maabara ya BioNTech na CureVac kuharakisha kazi yao kuhusu chanjo ya Corona na kuongeza uwezo wa uzalishaji nchini.
Berlin mwezi uliopita ilitenga fedha milioni 745 kwa maabara ya BioNTech na CureVac kuharakisha kazi yao kuhusu chanjo ya Corona na kuongeza uwezo wa uzalishaji nchini. REUTERS

Ujerumani inafanya maandalizi kuanza kampeni ya chanjo ya Corona kabla ya mwisho wa mwaka huu, Gazeti la Bild limeripoti leo Ijumaa, bila hata hivyo kutaja vyanzo.

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na gazeti la Bild, Wizara ya Afya imepanga kuweka vituo 60 vya kuhifadhi dawa itakayotumiwa kwa chanjo hiyo na kutaka majimbo yote ya nchi hiyo kuonyesha ifikapo Novemba 10 mahali pa kuweka vituo hivyo.

Waziri wa Afya Jens Spahn, ambaye mwenyewe aliambukizwa virusi vya Corona, alisema wiki hii kwenye mkutano kwa njia ya video kwamba maabara ya Ujerumani BioNTech iko karibu kupata kibali cha kuiruhusu kutoa chanjo yake, wamebaini washiriki walionukuliwa na Gazeti la Bild.

Alipoulizwa kuhusu ratiba ya utoaji wa chanjo ya kwanza, Spahn alijibu: "Chanjo dhidi ya Corona inaweza kutolewakabla ya mwisho wa mwaka," washiriki wameongeza.

BioNTech yatengeneza chanjo dhidi ya Corona kwa kushirikiana na Pfizer.

Berlin mwezi uliopita ilitenga fedha milioni 745 kwa maabara ya BioNTech na CureVac kuharakisha kazi yao kuhusu chanjo ya Corona na kuongeza uwezo wa uzalishaji nchini.

Ujerumani inakabiliwa na ongezeko la visa vipya vya maambukizi, baada ya visa vipya 10,000 kuthibitishwa siku ya Alhamisi.