ITALIA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Italia yakumbwa na maambukizi zaidi

Jimbo la Lombardy limeendelea kuwa jimbo lililooathirika zaidi, lilikwa na kesi 4,916 zilizothibitishwa
Jimbo la Lombardy limeendelea kuwa jimbo lililooathirika zaidi, lilikwa na kesi 4,916 zilizothibitishwa Shahzad ABDUL / AFP

Italia imerekodi visa vipya 19,143 vya maambukizi ya virusi vya Corona katika muda wa saa 24 zilizopita, kulingana na Wizara ya Afya, ikiwa ni rekodi mpya ya kila siku.

Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo jimbo la Campania, ambao ni pamoja na jiji la Naples, limetangaza upya masharti ya watu kutotembea kwa mwezi mmoja.

Idadi ya vifo vilivyoripotiwa Ijumaa katika wilaya hiyo ni 91, ikiwa ni idadi ya chini ikilinganishwa na vifo 136 vilivyorekodiwa siku ya Alhamisi, na mbali na idadi kubwa ya vifo vilivyoripotwa mwezi Machi na Aprili, ambapo watu zaidi ya 900 walifariki dunia kila siku.

Idadi ya visa vya maambukizi ambayo ilikuwa ilishuka katika majira ya Joto, imeongezeka mara saba tangu mwanzoni mwa mwezi Oktoba, na virusi vinasambaa kwa kasi kote nchini ikilinganishwa na mlipuko wa kwanza, huku jimbo la Lombardy likiendelea kuwa jimbo lililooathirika zaidi, lilikwa na kesi 4,916 zilizothibitishwa;

Campania, mkoa wa pili ulioathirika zaidi siku ya Ijumaa kwa visa 2,280 vya maambukizi, umetangaza hatua kagkaa kwa lengo la kupunguza kuenea kwa virusi hivyo, na kuomba nchi nzima kufanya hivyo.