UTURUKI-UFARANSA-USHIRIKIANO

Mvutano wa Ufaransa na Uturuki: Erdogan awataka raia wake kususia bidhaa za Ufaransa

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akiwahutubia wafuasi wa chama chake huko Malatya mashariki mwa Uturuki, Oktoba 25, 2020.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akiwahutubia wafuasi wa chama chake huko Malatya mashariki mwa Uturuki, Oktoba 25, 2020. Turkish Presidency via AP, Pool

Rais Recep wa Uturuki Tayyip Erdogan ametoa wito kwa Waturuki kususia bidhaa kutoka Ufaransa, katikati ya mzozo na Paris juu ya Waislamu wanavyochukuliwa nchini Ufaransa na baada ya kuenea kwa maandamano na wito kutoka nchi kadhaa za Kiarabu.

Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo kampuni kadhaa za Uarabuni zimeondoa bidhaa zake Ufaransa kutokana na kauli ya rais Emmanuel Macron dhidi ya vibonzo vya Mtume Muhammad.

Rais Macron alisema Ufaransa haitoacha kuchora vibonzo, kutokana na kuchinjwa kwa mwalimu Samuel Paty aliyewaonesha wanafunzi wake kibonzo cha Mtume Muhammad mapema mwezi huu, katika kitongoji kimoja cha Paris katika somo kuhusu uhuru wa kujieleza.

Siku ya Ijumaa vibonzo vya Mtume Muhammad vilichapishwa kwenye majengo ya serikali nchini Ufaransa, hatua iliyokasirisha nchi za Kiarabu.

"Kama vile huko Ufaransa wengine wanasema" usinunue bidhaa kutoka Uturuki ", hapa ninalihutubia taifa: ninawaomba, msusie bidhaa kutoka Ufaransa, msinunue," amesema Recep Tayyip Erdogan katika hotuba aliyoitoa Jumatatu hii, Oktoba 26 huko Ankara .

"Kampeni ya kuua watu kwa mawe sawa na ile dhidi ya Wayahudi wa Ulaya kabla ya Vita ya Pili ya Dunia inaendeshwa dhidi ya Waislamu," ameongeza, akiwashutumu viongozi wengine wa Ulaya 'wakifasti'.

Wito wa kususia bidhaa za Ufaransa unaendelea kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii.