UJERUMANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Zaidi ya visa vipya 11,000 vyathibitishwa nchini Ujerumani

Idadi ya visa vya virusi vya Corona nchini Ujerumani imekuwa ikipanda katika wiki za hivi karibuni.
Idadi ya visa vya virusi vya Corona nchini Ujerumani imekuwa ikipanda katika wiki za hivi karibuni. AFP/Torsten Silz

Idadi ya visa vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi vya Corona nchini Ujerumani imepanda hadi 449,275, baada ya visa vipya 11,409 kuthibitishwa, kulingana na takwimu iliyotolewa leo Jumanne na kituo cha kuzuia na kudhibiti magonjwa cha Robert Koch (RKI).

Matangazo ya kibiashara

Vifo vipya arobaini na mbili vimeripotiwa, na kufanya jumla ya vifo kufikia 10,098 tangu kuzuka kwa janga hilo hatari nchini Ujerumani.

Mlipuko wa virusi vya corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.