UJERUMANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Merkel ataka kufunga baa na mikahawa, kulingana na rasmu ya azimio

Angela Merkel pia anatarajia, wakati wa mkutano kwa njia ya video, kupata idhini kutoka kwa mawaziri-marais 16 ili kufunga kumbi za michezo, kumbi za filamu.
Angela Merkel pia anatarajia, wakati wa mkutano kwa njia ya video, kupata idhini kutoka kwa mawaziri-marais 16 ili kufunga kumbi za michezo, kumbi za filamu. REUTERS/Yves Herman

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel anatarajia kupata leo Jumatano idhni kutoka viongozi wa Majimbo 16 ya nchi hiyo kuhusu kufungwa kwa baa na migahawa yote kuanzia Novemba 4 ili kukabiliana na janga la Corona.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo kulingana na rasmu ya azimio, Angela Merkel anataka shule kuendelea na shughuli ya kuwapa elimu watoto.

Angela Merkel pia anatarajia, wakati wa mkutano kwa njia ya video, kupata idhini kutoka kwa mawaziri-marais 16 ili kufunga kumbi za michezo, kumbi za filamu na kumbi za maonyesho ya moja kwa moja, huku maduka yakisalia wazi kwa masharti ya kutekeleza hatua kali za usafi na kupunguza idadi ya wateja kwa wakati mmoja.

Hayo yanajiri wakati nchi nyingi barani Ulaya zimeendelea kurekodi idadi kubwa ya maambukizi, baada ya visa vipya kuripotiwa.

Ujerumani, ambayo ilichapisha viwango vya chini vya maambukizo kuliko nchi zingine kubwa wakati wa mlipuko wa kwanza wa janga hilo, sasa inakabiliwa na kuongezeka kwa kasi kwa idadi ya kesi mpya: takwimu zilizotolewa Jumatano zinaonyesha visa vipya 14,964 vya maambukizi katika muda wa saa 24, na kufanya idadi ya visa vya maambukizi kufikia 464,239, na vifo vifo 85 vya nyongeza. Tangu kuzuka kwa janga hilo, Corona imeua watu 10,098 katika nchi hii yenye watu wengi zaidi barani Ulaya (zaidi ya wakaazi milioni 83).

Mlipuko wa virusi vya corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.