UTURUKI-UFARANSA-USHIRIKIANO

Erdogan: Baadhi ya nchi zinataka 'kuanzisha vita vya kidini'

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, à Ankara, le 5 février 2020.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, à Ankara, le 5 février 2020. Adem ALTAN / AFP

Nchi za Magharibi zinazoushambulia Uislamu zinataka "kuanzisha vita vya kidini," rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema leo Jumatano wakati mvutano ukiendelea kuongezeka kati ya nchi yake na Ufaransa juu ya katuni za Mtume Muhammad.

Matangazo ya kibiashara

Katika hotuba yake kwa wabunge kutoka chama chake, AKP, kwenye makao makuu ya Bunge, rais wa Uturuki amesema kuwa mashambulio dhidi ya nabii huyo ni "suala la heshima kwetu".

Ankara hapo awali ilisema inazingatia "hatua zote muhimu za kisheria na kidiplomasia" baada ya kuchapishwa kwa katuni ya Recep Tayyip Erdogan kwenye ukurasa wa mbele wa Gazeti la Charlie Hebdo.

Nchi kadhaa za Kiislamu zimeedelea kupinga kauli ya rais wa Ufaransa kwamba nchi yake itaendelea kuchapisha katuni za Mtume Muhammad, katika kile alichosema ni uhuru wa kujieleza.