EU-CORONA-AFYA-UCHUMI

Umoja wa Ulaya wapendekeza hatua zaidi kwa vita dhidi ya Corona

Tume ya Ulaya imeshauri serikali kuratibu mikakati yao ya upimaji na kutumia zaidi upimaji maalumu hata kama mfumo wa aina hiyo unaonyesha dalili za mvutano.
Tume ya Ulaya imeshauri serikali kuratibu mikakati yao ya upimaji na kutumia zaidi upimaji maalumu hata kama mfumo wa aina hiyo unaonyesha dalili za mvutano. (Carte : D. Alpöge / RFI)

Tume ya Ulaya imependekeza mfululizo wa hatua mpya dhidi ya janga la COVID-19 katika bara la Ulaya kutokana na ongezeko la maambukizi mapya, ukitolea wito nchi 27 wanachama wa Umoja huo kuboresha uratibu wao.

Matangazo ya kibiashara

"Kulegeza masharti yaliyotumika wakati wa majira ya joto haikuendana na maamuzi yanayowezesha kuunda uwezo wa kutosha wa majibu", Tume kya Ulaya imebaini katika taarifa yake.

Tume ya Ulaya imeshauri serikali kuratibu mikakati yao ya upimaji na kutumia zaidi upimaji maalumu hata kama mfumo wa aina hiyo unaonyesha dalili za mvutano.

Tume ya Umoja wa Ulaya imeongeza kuwa "uhaba wa sasa katika uwezo wa kupima" unahitaji jibu la haraka.

Rais wa Tume ya Ulaya, Ursula von der Leyen, alitangaza wiki iliyopita kwamba Umoja wa Ulaya utatoa euro milioni 100 kununua vipimo milioni 22 vya antijeni ili kukidhi "mahitaji ya haraka" ya nchi wanachama lakini alitoa wito kwa nchi hizi wanachama wa Umoja wa Ulaya kwenda mbali zaidi kwa kutumia utaratibu wa ununuzi wa makundi.

Tume hiyo pia imependekeza kuanzisha sheria za kawaida juu ya vipimo vya lazima kwa wasafiri.

Nchi wanachama zinapaswa pia zisamehe vifaa vya vipimo na chanjo kutoka kwa VAT, amesema, akisisitiza wito wake kwa serikali kwa ufafanuzi wa haraka wa mikakati ya chanjo, ili watu walio katika mazingira magumu zaidi wapate haraka iwezekanavyo chanjo za baadaye dhidi ya COVID-19.

Kwa mujibu wa Ursula von der Leyen, chanjo zinaweza kupatikana Ulaya tangu mwanzoni mwa mwezi wa Aprili.