UJERUMANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Karibu visa vipya 17,000 vya maambukizi vyathibitishwa nchini Ujerumani

Idadi ya visa vya virusi vya Corona nchini Ujerumani imekuwa ikipanda katika wiki za hivi karibuni.
Idadi ya visa vya virusi vya Corona nchini Ujerumani imekuwa ikipanda katika wiki za hivi karibuni. Luftwaffe/Johannes Heyn/Handout via Reuters

Idadi ya visa vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi vya Corona nchini Ujerumani imepanda hadi 481,013, baada ya visa vipya zaidi ya 16,774 kuthibitishwa siku moja iliyopota, kulingana na takwimu zilizotolewa na kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa cha Robert Koch (RKI).

Matangazo ya kibiashara

Vifo zaidi ya themanini na tisa vimeripotiwa, na kufanya jumla ya vifo kufikia 10,272 tangu kuzuka kwa janga hilo nchini Ujerumani.

Ongezeko la visa vya maambukizi ya kila siku limeendelea kushuhudiwa katika nchi kadhaa za bara la Ulaya.

Wiki hii Tume ya Ulaya imependekeza mfululizo wa hatua mpya dhidi ya janga la COVID-19 katika bara la Ulaya kutokana na ongezeko la maambukizi mapya, ukitolea wito nchi 27 wanachama wa Umoja huo kuboresha uratibu wao.

Tume ya Ulaya imeshauri serikali kuratibu mikakati yao ya upimaji na kutumia zaidi upimaji maalumu hata kama mfumo wa aina hiyo unaonyesha dalili za mvutano.

Mlipuko wa virusi vya corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.