ITALIA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Italia kutangaza sheria ya kutotoka nje usiku lakini sio kizuizi

Italia inatarajia kuimarisha hatua zake kuhusu raia kutembea ili kuzuia kuenea kwa wimbi jipya la virusi vya Corona, bila hata kuchukuwa hatua ya kupiga tena marufuku raia kubaki katika majumba yao, Waziri Mkuu wa nchi hiyo Giuseppe Conte alitangaza leo Jumatatu.

Waziri Mkuu wa Italia Giuseppe Conte huko Brussels, Oktoba 16, 2020.
Waziri Mkuu wa Italia Giuseppe Conte huko Brussels, Oktoba 16, 2020. REUTERS/Johanna Geron
Matangazo ya kibiashara

Akiongea mbele ya wabunge, Waziri Mkuu wa Italia amesema kuwa kuongezeka kwa janga hilo "kumezuia wasiwasi mkubwa" na kwamba wodi za wagonjwa mahututi wa Corona katika mikoa 15 kati ya 20 ya nchi hiyo zitakuwa zimejaa ndani ya mwezi mmoja ikiwa hakuna hatua zitakazochukuliwa.

Idadi ya kila siku ya maambukizi nchini Italia imeongezeka mara kumi katika kipindi cha mwezi wa Oktoba na sasa visa30,000 vya maambukizi vinaripotiwa kwa siku kwa wastani.

Giuseppe Conte amebaini kwamba Italia itagawanywa katika kanda tatu kulingana na hali ya kiafya ya mikoa hiyo.

Shughuli ya kuingia na kutoka katika mikoa iliyoathirika zaidi zitapunguzwa kwa sababu za kitaalam, chuo kikuu, afya au dharura.

Katika ngazi ya kitaifa, sheria ya kutotoka nje usiku itatangazwa - na mikoa kadhaa tayari inaitumia - na serikali inaweza kuamua kufungwa kwa vituo vya kibiashara mwishoni mwa wiki hii na kupunguza idadi katika sekta ya usafiri wa umma hadi 50%.