AUSTRIA-USALAMA

Wawili waua katika shambulio la risasi Austria

Watu kadhaa waaliokuwa wamejihami kwa bunduki, ambao mmoja wao bado anatafutwa, walishambulia maeneo sita tofauti huko Vienna Jumatatu karibu na sinagogi katikati mwa mji mkuu wa Austria, na kuua watu wawili na angalau 14 wamejeruhiwa.

Mamlaka imetoa wito kwa wakaazi kukaa nyumbani na usafiri wa umma umekatishwa katikati mwa jiji.
Mamlaka imetoa wito kwa wakaazi kukaa nyumbani na usafiri wa umma umekatishwa katikati mwa jiji. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Kansela Sebastian Kurz amelitaja shambulio hilo kama "shambulio la kigaidi lenye kuchukiza".

Walioshuhudia wanasema washambuliaji walifyatua risasi dhidi ya umati wa watu waliokusanyika katika baa, kwani wengi walitumia fursa ya kujielekeza katika baa wakati wa usiku kabla ya kuanza kutumika amri ya kutotoka nje usiku kwa kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona.

Mmoja wa washukiwa aliuawa kwa kupigwa risasi na polisi, ambao kwa kiasi kikubwa walizingira kituo cha kihistoria cha Vienna na kuanza msako kuwatafuta washambuliaji wengine.

Mamlaka imetoa wito kwa wakaazi kukaa nyumbani na usafiri wa umma umekatishwa katikati mwa jiji.

"Ni siku ngumu zaidi kwa Austria kwa miaka mingi," Waziri wa Mambo ya Ndani Karl Nehammer amesema katika mkutano na waandishi wa habari.

Miongoni mwa watu waliojeruhiwa ni ni afisa wa polisi baada ya shambulizi hilo kutokea karibu na hekalu la kuabudu.

Polisi katika nchi jirani ya Jamhuri ya Czevch wameanziusha Operesheni ya kumsaka mshukiwa anayetafutwa huku rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akishtumu mashambulizi hayo.

Shambulizi hili limetokea saa chache tu kabla ya Austria kutangaza masharti mapya ya kupambana na janga la Corona, kutokana na ongezeko la virusi hivyo.