UJERUMANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Karibu kesi mpya 20,000 zathibitishwa nchini Ujerumani

Idadi ya kesi zilizothibitishwa za maambukizi ya Corona nchini Ujerumani zimeongezeka hadi 597,583, baada ya kesi mpya 19,990 kuripotiwa, kulingana na takwimu zilizotolewa leo Alhamisi na kituo cha kuzuia na kudhibiti magonjwa cha Robert Koch (RKI).

Idadi ya visa vya virusi vya Corona nchini Ujerumani imekuwa ikipanda katika wiki za hivi karibuni.
Idadi ya visa vya virusi vya Corona nchini Ujerumani imekuwa ikipanda katika wiki za hivi karibuni. Ina FASSBENDER / AFP
Matangazo ya kibiashara

Taasisi hiyo pia imeripoti vifo vipya 118, na kufanya idadi ya vifo kufikia 10,930 tangu kuzuka kwa janga hilo nchini Ujerumani.

Mlipuko wa virusi vya corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.