UINGEREZA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Uingereza yachukua tena hatua za watu kutotembea

Katika matumaini ya kuzuia kuenea kwa haraka kwa ugonjwa hatari wa COVID-19, Uingereza imechukuwa masharti mengine ya kupiga marufuku watu kutembea kwa muda wa mwezi mmoja.

Ulaya ndio eneo duniani ambapo virusi vya mlipuko mpya wa Corona vinasambaa haraka zaidi: zaidi ya kesi milioni 11 zimerekodiwa barani humo, nusu idadi hiyo ikiripotiwa nchini Urusi, Ufaransa, Uhispania na Uingereza.
Ulaya ndio eneo duniani ambapo virusi vya mlipuko mpya wa Corona vinasambaa haraka zaidi: zaidi ya kesi milioni 11 zimerekodiwa barani humo, nusu idadi hiyo ikiripotiwa nchini Urusi, Ufaransa, Uhispania na Uingereza. AFP
Matangazo ya kibiashara

Uingereza, nchini yenye wakaazi Milioni 56 inakabiliwa na maambukizi zaidi kutokana na mlipuko mpya wa virusi vya Corona.

Haya yanajiri wakati Italia na Kupro zinajiandaa kutangaza sheria ya kutotoka nje usiku, huku Marekani ikirekodi visa vipya 100,000 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Ulaya ndio eneo duniani ambapo virusi vya mlipuko mpya wa Corona vinasambaa haraka zaidi: zaidi ya kesi milioni 11 zimerekodiwa barani humo, nusu idadi hiyo ikiripotiwa nchini Urusi, Ufaransa, Uhispania na Uingereza.

Janga hilo limewauwa watu wasiopungua milioni 1.2 duniani, idadi kubwa ya vifo inaripotiwa Marekani kwa vifo zaidi 233,650. Nchi hiyo pia ilirekodi 99,660 mpya za maambukizi Jumatano wiki hii.

Baada ya Ireland na Ufaransa, Uingereza imechukuwa hatua ya kupiga marufu raia wake Milioni 56 kutotembea kwa kipindi cha mwezi mmoja.

Mlipuko wa virusi vya corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa Covid-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.