URENO-CORONA-AFYA

Coronavirus: Ureno kutangaza sheria ya kutotoka nje kuanzia Jumatatu

Waziri Mkuu wa Ureno, Antonio Costa.
Waziri Mkuu wa Ureno, Antonio Costa. Foto: Reuters/Rafael Marchante

Hali ya dharura ya kiafya ambayo itaanza kutumika Jumatatu nchini Ureno itahusu sehemu kubwa ya nchi hiyo na itaambatana na sheria ya kutotoka nje usiku kwa angalau wiki mbili, Waziri Mkuu Antonio Costa ametangaza.

Matangazo ya kibiashara

"Marufuku haya ya kutotembea kwenye barabara za umma" itatumika katika wilaya 121, ambazo ziko chini ya kizuizi kipya tangu Jumatano na ambapo karibu 70% ya Wareno wanaishi, amesema Bwana Costa baada ya kikao cha dharura cha Baraza la mawaziri.

Hatua hii inakuja baada ya nchi hii ,a hasa nchi nyingi barani Ulaya kushuhudia ongezeko kubwa la maambukizi ya virusi vya Corona.

Wiki hii shirika la Afya Dunia, WHO, imeonya juu ya mlipuko wa janga hatari katika bara la Ulaya.

Bara la Ulaya sasa lina zaidi ya visa vya milioni 12 vya maambukizi ya virusi vya Corona kwa vifo karibu 300,000, ikiwa ni pamoja na Urusi. Shirika la Afya Duniani, WHO, limeonya kuwa wiki chache zijazo hali itakuwa ngumu zaidi.

WHO inasisitiza uvaaji wa barakoa na inatoa wito kwa shule kufunguliwa.