UFARANSA-MACRON-SIASA

Miaka 50 baada ya kifo cha Charles de Gaulle, Emmanuel Macron afanya ziara Colombey

Jenerali de Gaulle alifariki dunia miaka hamsini iliyopita. Alifariki dunia nyumbani kwake huko Colombey-les-deux-Églises, ambapo Emmanuel Macron amechagua kwenda kusherehekea kumbukumbu ya yule ambaye ameendelea kuwa mfano kwa viongozi wote wa Ufaransa kwa miongo kadhaa.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akipita karibu na sanamu la Jenerali de Gaulle kwenye makavazi ya Agizo la Ukombozi, Juni 18, 2020.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akipita karibu na sanamu la Jenerali de Gaulle kwenye makavazi ya Agizo la Ukombozi, Juni 18, 2020. Yoan Valat, Pool via AP
Matangazo ya kibiashara

Ni hatua ya mwisho ya maadhimisho ya mwaka wa de Gaulle uliyoandaliwa na rais wa Jamhuri. Rais Macron anatarajia kutoa heshima zake kwenye kaburi la Jenerali huyo ambaye atakumbukwa kwa miaka yote na wananchi wa Ufaransa.

Miaka 50 iliyopita, rais Georges Pompidou ndiye ambaye alitangaza kifo cha Jenerali de Gaulle akitangaza: "Jenerali de Gaulle amefariki dunia, Ufaransa imebaki mjane".

Huko London, pamoja na Prince Charles, Emmanuel Macron alisherehekea maadhimisho ya kumbukumbu ya mtu aliyetoa wito Juni 18, akiwataka wananchi wa Ufaransa kupitia kituo cha BBC, kujiunga naye na kupigania Ufaransa dhidi ya utawala wa Kifashisti.

"Mimi, Jenerali de Gaulle, ninawatolea wito wananchi wote wa Ufaransa ambao wanataka kuwa huru kunisikiliza na kunifuata".

Rais wa Ufaransa anataka kufuata nyayo za Jenerali de Gaulle kwa kuendeleza uzalendo na kutia mbele maslahi ya Ufaransa na Wafaransa.