UFARANSA-USALAMA

Ufaransa: Mabaki ya Maurice Genevoix yapelelwa katika makavazi ya kitaifa

Mabaki ya Maurice Genevoix, mwandishi maarufu wakati wa vita vya kwanza vya dunia (1914-1918) na mashujaa wengine katika vita hivyo yamepelekwa katika makumbusho ya kitaifa ya Panthéon.

Jeneza la Maurice Genevoix linawasili mbele ya makavazi ya kitaifa ya Pantheon, Novemba 11, 2020.
Jeneza la Maurice Genevoix linawasili mbele ya makavazi ya kitaifa ya Pantheon, Novemba 11, 2020. Christian Hartmann, Pool via AP
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, amekuwa akiwaongoza raia wa nchi yake kuwakumbua wanajeshi wa taifa hilo waliopigana na wengine kuangamia katika vita vya kwanza na vya pili vya dunia.

Rais Macron aliweka shada la maua katika kaburi la mwanajeshi ambaye hakufahamika huku akiwasha mwenge katika mnara maalum uliojengwa kuwakumbuoka wanajeshi hao.

"Hii ni kama njia mojawapo ya kutambua mchango watu mbalimbali walioshiriki katika kusaidia kumalizika kwa vita hivyo, " alisema rais wa Ufaransa.

Baada ya kumalizika kwa vita vya kwanza miaka 102 iliyopita, watu wengine walioenziwa ni pamja na mtunzi wa muziki Pascal Dusapin na Anselm Kiefer, mchoraji kutoka Ujerumani, ambao minara yao imetengezwa.

Maadhimisho ya mwaka huu yalihudhuriwa na watu wachache kutokana na janga la virusi vya Corona.