Visa vya maambuziki vyaongezeka Ukraine, rais alazwa hospitali
Rais wa Ukraine Volodimir Zelensky amelazwa hospitalini baada ya kuambukizwa virusi vya Corona, vyombo vya habari vya nchini Ukraine vimeripoti leo Alhamisi, wakati Ukraine imerekodi idadi kubwa ya maambukiz ya kila siku.
Imechapishwa:
Hakuna uthibitisho ulioweza kupatikana kutoka kwa wasaidizi wake. Rais Zelensky, ambaye ana umri wa miaka 42, madarakani tangu Mei 2019, aliambukizwa mapema wiki hii, vyombo vya habari vya Ukraine vimeongeza vikinukuu chanzo kutoka ikulu.
Takwimu kutoka Wizara ya Afya zinaonyesha visa vipya 11,057 vya maambukizi ya virusi vya Corona katika muda wa saa 24. Rekodi ya awali (10,746) ni ya tarehe 7 Novemba.
Wakati huo huo, nchi hiyo imerekodi vifo vipya 198 kutokana na virusi vya Corona.Tangu kuzuka kwa virusi vya Corona nchini Ukraine, watu 500,865 wameambukizwa virusi hivyo na kusababisha vifo watu 9,145.