UINGEREZA-EU-USHIRIKIANO

Mazungumzo kuhusu Brexit kuanza tena Jumatatu

Mazungumzo kati ya Uingereza na Umoja wa Ulaya juu ya uhusiano wao wa baadaye yataanza tena Jumatatu wiki ijayo, na pande hizo mbili bado hazijaweza kukubaliana juu ya masuala ya uvuvi na sheria za ushindani ya haki wiki saba tu kabla ya tarehe yao ya mwisho ya mazungumzo.

Kambi zote mbili zinasema zinataka kufikia makubaliano kabla ya Desemba 31.
Kambi zote mbili zinasema zinataka kufikia makubaliano kabla ya Desemba 31. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Kambi zote mbili zinasema zinataka kufikia makubaliano kabla ya Desemba 31, muda wa mwisho wa kumalizika kwa kipindi cha mpito kufuatia Uingereza kujiondoa katika Umoja wa Ulaya, lakini hadi sasa maendeleo kidogo yamepatikana, London inasisitiza hasa juu ya ya kuhifadhiwa kwa uhuru wake.

"Mazungumzo yanaendelea London leo; kutakuwa na mapumziko mwishoni mwa wiki hii na kisha tunatarajia mazungumzo kuanza tena Jumatatu huko Brussels," msemaji wa Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amewaambia waandishi wa habari leo Ijumaa.

"Timu za mazungumzo zinafanya kazi kwa bidii ili kuziba pengo kubwa kati yetu. Kwa upande wetu, tunaendelea kutafuta suluhisho ambazo zinaheshimu kabisa uhuru wa Uingereza, lakini matatizo bado yapo, pamoja na sheria za ushindani katika masuala ya haki na uvuvi, ”amesema.

Alipoulizwa ikiwa kuondoka kwa Dominic Cummings, mshauri maalum wa Boris Johnson juu ya Brexit, kunaweza kuonyesha kwamba London italegeza msimamo wake juu ya suala hilo, msemaji huyo amesema: "Msimamo wa serikali [...] haubadiliki. "