UJERUMANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Ujerumani yarekodi visa vipya 14,000

Idadi ya visa vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi vya Corona nchini Ujerumani imepanda hadi 815,746, baada ya visa vipya 14,419 kuripotiwa siku moja kabla, kulingana na takwimu zilizotolewa leo Jumanne na kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa cha Robert Koch (RKI.

Berlin mwezi uliopita ilitenga fedha milioni 745 kwa maabara ya BioNTech na CureVac kuharakisha kazi yao kuhusu chanjo ya Corona na kuongeza uwezo wa uzalishaji nchini.
Berlin mwezi uliopita ilitenga fedha milioni 745 kwa maabara ya BioNTech na CureVac kuharakisha kazi yao kuhusu chanjo ya Corona na kuongeza uwezo wa uzalishaji nchini. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Taasisi hiyo pia imekodi vifo vipya 267, na kufanya idadi ya vifo kufikia 12,814 tangu kuzuka kwa janga hilo nchini Ujerumani.

Ulaya inaendelea kukabiliwa na maambukizi mapya kufuatia mlipuko mpya wa COVID-19. Nchi kadhaa barani Ulaya zimerejesha upya hatua kadhaa zilizochukuliwa wakati wa mlipuko wa kwanza, tangu ugonjwa huo kuzuka huko Wuhan, mwichoni mwa mwezi Desemba mwaka jana nchini China.

Wiki mbili zilizopita shirika la Afya Dunia, WHO, lilionya juu ya mlipuko wa janga hatari katika bara la Ulaya.

Bara la Ulaya sasa lina zaidi ya visa vya milioni 12 vya maambukizi ya virusi vya Corona kwa vifo zaidi ya 300,000, ikiwa ni pamoja na Urusi. Shirika la Afya Duniani, WHO, lilionya kuwa wiki chache zijazo hali itakuwa ngumu zaidi.

WHO inasisitiza uvaaji wa barakoa na inatoa wito kwa shule kufunguliwa.