EU-POLAND-HUNGARY-UCHUMI

Hungary na Poland waweka pingamizi kwa bajeti mpya ya Ulaya

Spika wa Bunge la Ulaya David Sassoli.
Spika wa Bunge la Ulaya David Sassoli. . REUTERS/Francois Lenoir

Wakati serikali za Umoja wa Ulaya kwa kiasi kikubwa zimeanza kuarifu Tume ya Ulaya miradi ambayo wanakusudia kufadhili kwa mpango wa kufufua uchumi wa umoja huo, tayari mpango huo unakabiliwa na tishio.

Matangazo ya kibiashara

Poland na Hungary wameweka pingamizi baada ya mpango huo wa euro milioni 750 kuwa mada ya mapatano ya baada ya mkutano wa siku nne, mwezi Julai mwaka huu.

Pingamizi hii ya Hungary na Poland kwa bajeti ya Ulaya sio jambo la kushangaza sana, lakini inabaki ni jukumu la wajumbe wakuu kutoka bunge la Ulaya katika mazungumzo hayo, ikiwa ni pamoja na Ujerumani ambayo, ambayo inaongoza baraza la nchi wanachama 27 kwa miezi sita. Walikuwa walitangaza kwamba wamefikia maelewano Jumanne iliyopita baada ya mazungumzo marefu.

Maelewano haya (ambayo yanaongeza bajeti ya Umoja wa Ulaya kwa zaidi ya miaka saba kwa euro bilioni 17) sasa yanakabiliwa na tishio.

Awali Poland iilisema kuwa itazuia uidhinishaji wa bajeti mpya ya Umoja wa Ulaya iwapo kutolewa kwa fedha za umoja huo kutafungamanishwa na masharti ya kuitaka nchi hiyo kuheshimu misingi ya utawala wa sheria.

Akizungumza na kituo kimoja cha redio, kiongozi wa ofisi ya waziri mkuu wa Poland Michal Dworczyk alisema iwapo Umoja wa Ulaya utakiuka mikataba na maamuzi yaliyofikiwa na wakuu wa mataifa ya nchi wanachama, Poland haitaridhia kupitishwa kwa bajeti ya kanda hiyo.

Poland na Hungary zinapinga vikali kuanzishwa masharti ya kutolewa kwa fedha za bajeti za Umoja wa Ulaya na zimedai kuwa zilizuia majaribio kadhaa ya kutungwa kanuni za aina hiyo kwenye mkutano wa kilele wa kanda hiyo mwezi Julai.