WHO-CORONA-AFYA

Idadi ya maambukizi yapungua kwa mara ya kwanza Ulaya

Bara la ulaya limeendelea kushuhudia visa vingi vya maambukizi ya Corona.
Bara la ulaya limeendelea kushuhudia visa vingi vya maambukizi ya Corona. © Czarek Sokolowski / AP Photo

Takwimu za shirika la Afya Duniani, WHO, zinaonesha kuwa idadi ya maambukizi ya virusi vya Covid-19 barani Ulaya ilipungua wiki iliyopita kwa mara ya kwanza baada ya miezi mitatu, lakini idadi ya vifo iliendelea kuongezeka.

Matangazo ya kibiashara

Kufikia mwishoni mwa wiki iliyopita, watu karibu Milioni nne walikuwa wameambukizwa virusi hivyo kote duniani, huku wengine karibu Elfu Sitini wakiwa wamepoteza maisha.

Barani Ulaya pekee, kufikia siku ya Jumanne wiki hii, idadi ya maambukizi iliongezeka na kufikia zaidi ya Milioni 15 na kusalia eneo ambalo limeathiriwa pakubwa na janga la Covid-9.

Licha ya bara la Ulaya wiki iliyopita kushuhudia maambukizi mapya Milioni Moja na Laki Nane, Shirika la Afya Duniani, WHO, limesema kiwango cha maambukizi, kilipungua kwa asilimia 10.

Idadi ya vifo iliyoripotiwa wiki iliyopita barani Ulaya ilikuwa ni Elfu 29, ambalo ni sawa na ongezeko asilimia 18.

Mataifa kadhaa barani Ulaya yamezuia raia wake kutembea, wakati huu idadi ya maambukizi duniani ikifikia zaidi ya Elfu 55 na wengine Milioni Moja na Laki tatu wamepoteza maisha.