EU-POLAND-HUNGARY-UCHUMI

Mpango wa kuinua uchumi wa Umoja wa Ulaya waendelea kukwama

Taasisi za Ulaya bado hazijaidhinisha mpango wa kufufua uchumi. Hungary na Poland zinakataa mfumo kuhusu ulinzi wa utawala wenye sheria.

Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban na mwenzake wa Poland Mateusz Morawiecki kwenye mkutano na waandishi wa habari huko Lublin, Poland, Septemba 11, 2020.
Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban na mwenzake wa Poland Mateusz Morawiecki kwenye mkutano na waandishi wa habari huko Lublin, Poland, Septemba 11, 2020. AP Photo/Czarek Sokolowski
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban amesema ana matumaini kuwa suluhu kuhusu bajeti ya Umoja wa Ulaya inayolenga kuinua uchumi wa umoja huo itapatikana.

Orban ameyasema hayo baada ya Hungary na Poland kupiga kura ya turufu kukataa kuunga mkono mpango wa kifedha kwa ajili ya wanachama wote wa Umoja wa Ulaya, licha ya kuwa wao ndio wanaofadhiliwa kwa kiwango kikubwa.

Hata hivyo fedha hizo zina masharti ya kuheshimu utawala wa sheria.

Waziri mkuu huyo wa Hungary amesema huenda kukawa na mapendekezo kadhaa ya kuutatua mkwamo huo ambapo masuala ya kisheria ndio yataamua na sio kwa njia za kisiasa.