UJERUMANI-MERKEL-SIASA

Ujerumani: Kansela Angela Merkel atimiza miaka 15 madarakani

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amekuwa madarakani kwa miaka 15, rekodi ya maisha marefu ya kisiasa nchini.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amekuwa madarakani kwa miaka 15, rekodi ya maisha marefu ya kisiasa nchini. REUTERS - POOL

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel aliingia madarakani Novemba 22, 2005. Miezi miwili baada ya uchaguzi mkuu, Angela Merkel alichaguliwa kuwa Kansela kwa mara ya kwanza akiwa kiongozi wa muungano mkubwa wa vyama vya siasa.

Matangazo ya kibiashara

Wakati huo, hakuna mtu alikuwa na uhakika kuwa kiongozi mpya wa ujerumani atakuwa madarakani kwa muda mrefu kiasi hicho.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, ambaye umaarufu wake umepunguwa tena tangu kuzuka kwa mgogoro wa kiafya na kiuchumi, hivi karibuni alisema kuwa hana nia ya kubadili uamuzi wake na kwamba muhula wake wa sasa utakuwa wa mwisho.

Angela Merkel ameongoza serikali ya shirikisho nchini Ujerumani tangu mwaka 2005.

Kufuatia uchaguzi wa mwisho wa wabunge mwezi Septemba 2017, ambao ulionyesha jinsi gani kambi yake ya Conservative CDU-CSU iligawanyika na kupoteza umaarufu.

Merkel aliingia katika siasa na kuwa kama msemaji wa waziri mkuu wa mwisho katika iliyokuwa Ujerumani Mashariki, Lothar de Maiziere, wakati huo akiwa na umri wa miaka 35.

Chini ya Kansela Helmut Kohl mwaka 1994 alikuwa waziri wa mazingira na usalama wa nyuklia, wizara muhimu kabisa kwa mtu anayeshikilia shahada ya uzamifu katika fizikia.

Baada ya kushindwa Helmut Kohl katika uchaguzi mkuu wa mwaka 1998, chama cha CDU kilipata mshtuko mkubwa lakini sio kwa Merkel, ambaye aliitumia nafasi yake barabara na mwaka 2000 akachaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho.

Tangu mwaka 2008 Kansela Angela Merkel amekuwa akiangaliwa kimsingi kama kiongozi mzuri katika kukabiliana na migogoro. Katika suala la Ugiriki, alisaidia kuikowa sarafu ya euro.

Haijapata kutokea katika historia ya Ujerumani baada ya mwaka 1945 kutokea mwanasiasa aliyewekewa matumani kidogo kama ilivyotokea kwa binti huyo wa mchungaji kutoka Mashariki.

►Soma zaidi: Angela Merkel: Huu ndio muhula wangu wa mwisho