ULAYA-WHO-CORONA-AFYA

Coronavirus: WHO yaonya nchi za Ulaya kuchukuwa hatua madhubuti dhidi ya COVID-19

Mlipuko wa virusi vya Corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.
Mlipuko wa virusi vya Corona unaosababisha ugonjwa wa Covid-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019. NEXU Science Communication/via REUTERS

Shirika la Afya Duniani, WHO, linaonya kuwa huenda kukatokea na mlipuko wa tatu wa COVID-19 barani Ulaya, iwapo serikali zitashindwa kuweka mikakati inayohitajika kama ilivyokuwa, kuzuia mlipuko wa pilli.

Matangazo ya kibiashara

Mjumbe wa WHO kuhusu maambukizi ya COVID-19, David Nabarro, ameonya kuwa mlipuko huo huenda ukashuhudiwa mapema mwaka 2021, iwapo hatua madhubuti hazitachukuliwa kudhibiti mlipuko mpya.

Nabarro ameliambia Gazeti nchini Uswisi kuwa mataifa mengi barani Ulaya, yameshindwa kuweka miundombinu inayohitajika kuzuia mlipuko wa pili na hivyo ametaka mataifa hayo kujipanga mapema.

Kauli yake imekuja wakati huu bara la Ulaya likishuhudia idadi ya maambukizi kushuka katika baadhi ya lakini Ujerumani na Ufaransa zimeandikisha ongezeko la maambukizi Elfu 33.

Aidha, ameonya kuwa Uswisi huenda ikashuhudia ongezeko kubwa la vifo na maambukizi, huku akiyataka mataifa ya Ulaya kuiga mfano wa nchi kama Korea Kusini ambayo ina maambukizi machache kutokana na raia wake kufuata kanuni za afya za kujitenga, kunawa mikono na kuvaa barakoa kila wakati.