UJERUMANI-CORONA-AFYA

Ujerumani yajiandaa kwa vizuizi dhidi ya Corona hadi Desemba 20

Novemba 2 Ujerumani ilitangaza sehemu ya makataa kwa mwezi mmoja ili kudhibiti wimbi jipya la janga la COVID-19 linaloendelea kuathiri sehemu kubwa ya Ulaya, lakini idadi ya maambukizi haipunguki.
Novemba 2 Ujerumani ilitangaza sehemu ya makataa kwa mwezi mmoja ili kudhibiti wimbi jipya la janga la COVID-19 linaloendelea kuathiri sehemu kubwa ya Ulaya, lakini idadi ya maambukizi haipunguki. REUTERS

Ujerumani inaweza kuongeza makataa dhidi ya kusambaa kwa virusi vya Corona na kuongeza muda wa hatua za kudhibiti ugonjwa COVID-19 hadi Desemba 20, kulingana na baadhi ya wanasiasa na pendekezo la rasimu ambalo shirika la habari la Reuters limepata kopi.

Matangazo ya kibiashara

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel anatarajia kufanya mazungumzo Jumatano na viongozi wa majimbo (Länder) kumi na sita ya nchi hiyo Jumatano wiki hii.

Novemba 2 Ujerumani ilitangaza sehemu ya makataa kwa mwezi mmoja ili kudhibiti wimbi jipya la janga la COVID-19 linaloendelea kuathiri sehemu kubwa ya Ulaya, lakini idadi ya maambukizi haipunguki.

"Vitu vingi vinaonyesha kwamba vizuizi vya sasa lazima viongezwe muda zaidi , hadi Novemba 30," Waziri wa Fedha Olaf Scholz ameliambia Gazeti la Bild am Sonntag (BamS).

Baa na mikahawa vimefungwa, lakini shule na maduka yamebaki wazi. Mikusanyiko ya watu binafsi imezuiliwa kwa kiwango cha juu cha watu 10 kutoka kwa familia mbili tofauti. Kulingana na pendekezo la rasimu, idadi hii inaweza kupunguzwa hadi watu watano.