UJERUMANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Idadi ya vifo nchini Ujerumani yazidi 940,000

Hospitali inayohudumia wagonjwa wa Corona iliyoanzishwa katika Kituo cha Maonyesho cha Berlin, picha iliyopigwa Aprili 23, 2020.
Hospitali inayohudumia wagonjwa wa Corona iliyoanzishwa katika Kituo cha Maonyesho cha Berlin, picha iliyopigwa Aprili 23, 2020. © AFP

Idadi ya visa vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi vya Corona nchini Ujerumani imepanda hadi 942,687, baada ya visa vipya zaidi ya 13,554 kuripotiwa siku moja iliyopita, kulingana na takwimu zilizotolewa leo Jumanne na kituo cha kuzuia na kudhibiti magonjwa cha Robert Koch (RKI).

Matangazo ya kibiashara

Kituo hiki pia kimeripoti vifo vipya 249, na kufanya idadi ya walifariki dunia kufikia 14,361 tangu kuzuka kwa janga hilo nchini Ujerumani.

Kutokana na kuongezeka kwa visa vya maambukizi, Ujerumani inaajiandaa kwa vizuizi dhidi ya Corona hadi Desemba 20 Ujerumani inaweza kuongeza makataa dhidi ya kusambaa kwa virusi vya Corona na kuongeza muda wa hatua za kudhibiti ugonjwa COVID-19 hadi Desemba 20, kulingana na baadhi ya wanasiasa na pendekezo la rasimu ambalo shirika la habari la Reuters lilipata kopi mapema wiki hii.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel anatarajia kufanya mazungumzo Jumatano na viongozi wa majimbo (Länder) kumi na sita ya nchi hiyo Jumatano wiki hii.

Novemba 2 Ujerumani ilitangaza sehemu ya makataa kwa mwezi mmoja ili kudhibiti wimbi jipya la janga la COVID-19 linaloendelea kuathiri sehemu kubwa ya Ulaya, lakini idadi ya maambukizi haipunguki.

"Vitu vingi vinaonyesha kwamba vizuizi vya sasa lazima viongezwe muda zaidi , hadi Novemba 30," Waziri wa Fedha Olaf Scholz ameliambia Gazeti la Bild am Sonntag (BamS).

Baa na mikahawa vimefungwa, lakini shule na maduka yamebaki wazi. Mikusanyiko ya watu binafsi imezuiliwa kwa kiwango cha juu cha watu 10 kutoka kwa familia mbili tofauti. Kulingana na pendekezo la rasimu, idadi hii inaweza kupunguzwa hadi watu watano.