UJERUMANI

Coronavirus: Zaidi ya watu milioni moja waambukizwa nchini Ujerumani

Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, hapa akiwa Berlin, tarehe 28 octobre 2020.
Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, hapa akiwa Berlin, tarehe 28 octobre 2020. Fabrizio Bensch/pool photo via AP

Idadi ya visa vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi vya Corona nchini Ujerumani imepanda hadi 1,006,394, baada ya visa vipya zaidi ya 22,806 kuthibitishwa siku moja iliyopita, kulingana na takwimu zilizotolewa leo Ijumaa na kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa cha Robert Koch (RKI).

Matangazo ya kibiashara

Kituo hiki pia kimebaini kwamba vifo vipya 426 vimeripotiwa, na kufanya idadi ya vifo kufikia 15,586 tangu kuzuka kwa janga hilo nchini Ujerumani.

 

Kutokana na kuongezeka kwa visa vya maambukizi, Ujerumani imekuwa inajiandaa kwa vizuizi dhidi ya Corona hadi Desemba 20.

 

Vitu vingi vinaonyesha kwamba vizuizi vya sasa lazima viongezwe muda zaidi , hadi Novemba 30," Waziri wa Fedha Olaf Scholz aliliambia Gazeti la Bild am Sonntag (BamS) mapema wiki hii.

Baa na mikahawa vimefungwa, lakini shule na maduka yamebaki wazi. Mikusanyiko ya watu binafsi imezuiliwa kwa kiwango cha juu cha watu 10 kutoka kwa familia mbili tofauti.

Mlipuko wa virusi vya corona unaosababisha ugonjwa wa COVID-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa COVID-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.