AZERBAIJAN-UFARANSA

Nagorno-Karabakh: Azerbaijan yainyooshea kidole cha lawama Ufaransa

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, hapa ilikuwa October 29, 2020.
Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, hapa ilikuwa October 29, 2020. Eric Gaillard/Pool via AP

Kulingana na makubaliano ya usitishaji wa mapigano yaliyofikiwa Novemba 9, Azerbaijan inachukuwa leo Jumanne Desemba 1 umiliki wa wilaya ya Lachin iliyokabidhiwa Armenia.

Matangazo ya kibiashara

Hayo yanajiri wakati mamlaka nchini Azerbaijan imeishtumu Ufaransa kubadili msimamo kuhusiana na suala hilo.

 

Azimio lililopitishwa na baraza la Seneti ya Ufaransa wiki iliyopita lilisababisha mvutano nchini Azerbaijan. Nakala hii ya kiishara, ambayo haina nguvu yoyote, imeomba kutambuliwa kwa Jamhuri ya Nagorno-Karabakh.

 

Maseneta, ambao walipitisha azimio hilo kwa idadi kubwa ya kura 305 dhidi ya 1, walichukua msimamo mkali kuhusu suala hili lenye lenye utata mkubwa katika kanda hiyo, suala ambalo bado halijapatiwa suluhisho.

 

Kutambua Nagorno-Karabakh kama eneo uhuru itakuwa sawa na kujiondoa kwenye nafasi ya kutoegemea upande wowote, msimamo ambao Ufaransa ulikuwa nao kwa miaka kadhaa katika mfumo wa kundi la Minsk, ambapo Ufaransa, Marekani na Urusi, zina jukumu la kutafutia ufumbuzi mgogoro kati ya Armenia na Azerbaijan.