UFARANSA

Rais wa zamani wa Ufaransa, Valéry Giscard d'Estaing, afariki dunia

Rais wa zamani wa Ufaransa, Valéry Giscard d'Estaing, hapa ilikuwa mwaka 2015.
Rais wa zamani wa Ufaransa, Valéry Giscard d'Estaing, hapa ilikuwa mwaka 2015. AP Photo/Pavel Golovkin

Rais wa zamani wa Ufaransa, Valéry Giscard d'Estaing, kati ya mwaka 1974 hadi 1984, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 94.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa familia yake, Giscard d'Estaing, alifariki kutokana na changamoto wa kupumua zilizosababishwa na maambukizi ya Covid 19.

Mwanasiasa huyu aliyekuwa na msimamo wa katim aliyeunga mkono umoja wa Ulaya na pia kupitisha sheria kuhusu masuala ya kuachana katika ndoa, kuruhusu utoaji mimba na matumizi ya dawa za uzazi wa mpango, ni miongoni mwa masuala yaliyompa umaarufu wakati wa utawala wake wa miaka 7.

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, amesema utawala wake uliibadilisha Ufaransa na bado sera zake nyingi zimeendelea kusaidia mabadiliko.

“Alikuwa mtumishi wa uma, mwanasiasa wa maendeleo na uhuru, kifo chake kimeitumbukiza Ufaransa katika majonzi,” ilisema taarifa ya rais Macron.

Familia yake tayari imesema Valéry Giscard d'Estaing, atazikwa kwa kuzingatia masharti ya kiafya na katika shughuli itakayofanyika kwa usiri.

Maisha yake Kisiasa

Baada ya kustaafu, Giscard d'Estaing, alipenda kujionesha kama mzee wa siasa za Ufaransa. Kama moja ya marais vijana, aliingia madarakani akiwa na umri wa miaka 48, ambapo alikuwa na maisha mazuri kisiasa kuliko hata wakati alipokuwa katika ikulu ya Elysee.

Wengi walimuona kama kiongozi mkorofi, ambapo urais wake ulifikia ukomo katika muda mfupi sana ambapo aling’olewa madarakani na vyama vya upinzani vya mrengo wa kushoto na kulia.

Pia wakati mmoja alijikuta katika kashfa ya kuwasaidia marais wa Afrika ambao walikuwa ni watawala wa kiimla.

Valéry Marie René Georges Giscard d'Estaing, alizaliwa tarehe 2 ya mwezi February mwaka 1926 kwenye mji wa Koblenz, moja ya maeneo yaliyowahi kutawaliwa na Ujerumani.

Baba yake alikuwa mtumishi wa uma na alifanya kazi katika vikosi vya Serikali, wakati mama yake alikuwa katika vuguvugu la mapinduzi ambalo liliushika mji wa Paris mwaka 1994.

Alifanya kazi kama mwalimu kwenye mji wa Montreal, kabla ya kupata shahada ya masuala ya utawala katika chuo kikuu cha Ufaransa.

Giscard d'Estaing, alimanusura afanikiwe kumshinda Mjamaa, François Mitterrand, katika duru ya pili ya uchaguzi kwa asili,ia 50.7, na kuwa raia wa kwanza kijana katika historia ya taifa la Ufaransa.