UFARANSA

Kifo cha Valéry Giscard d'Estaing: Emmanuel Macron atangaza siku ya maombolezo ya kitaifa

Rais wa zamani wa Ufaransa, Valery Giscard d'Estaing, mke wake, Anne-Aymone, pamoja na rais wa zamania Nicolas Sarkozy na Francois Hollande.
Rais wa zamani wa Ufaransa, Valery Giscard d'Estaing, mke wake, Anne-Aymone, pamoja na rais wa zamania Nicolas Sarkozy na Francois Hollande. Francois Mori/Pool via REUTERS

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametangaza Jumatano wiki ijayo kama siku ya maombolezo ya kitaifa kuhusiana na kifo cha rais wa zamani wa nchi hiyo Valéry Giscard d'Estaing, aliyefariki Jumatano wiki hii.

Matangazo ya kibiashara

Katika hotuba kwa taifa, rais Emmanuel Macron alimtaja Valéry Giscard d'Estaing kama "kiungo muhimu katika historia ya Jamhuri yetu. "

Valéry Giscard d'Estaing alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 94.

Rais Macron amebaini kwamba rais wa zamani na familia yake hawakutaka, "kwa sababu zisizozuilika", mazishi ya kitaifa kwa kiongozi huyo wa zamani kama yale yaliyoandaliwa kwa hayati Jacques Chirac mnamo mwaka wa 2019.

"Tarehe 2 Februari, siku ya kuzaliwa kwake, heshima za mwisho zitatolewa kwa Valéry Giscard d'Estaing katika makao makuu ya Bunge la Ulaya huko Strasbourg, ”ameongeza rais Macron.

Mazishi Valéry Giscard d'Estaing yatafanyika Jumamosi tarehe 5 Desemba huko Authon (Loir-et-Cher), ambapo kunapatikana makazi yake. Mazishi hayo yatahusdhuriwa na watu wadogo kutoka famlilia yake pamoja na viongozi wa kadhaa wa nchi.