UFARANSA-COVID19

Ufaransa kutoa chanjo ya Corona bure

Waziri mkuu wa Ufaransa, Jean Castex.
Waziri mkuu wa Ufaransa, Jean Castex. Ludovic Marin/Pool via REUTERS

Serikali ya Ufaransa imetangaza kuwa itaanza kuwapa chanjo ya kuzuia maambukizi ya Corona watu Milioni Moja kuanzia mwezi Januari, huku wengine Milioni 14 wakipata chanjo hiyo kuanzia mwezi Februari.

Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu Jean Castex amesema chanjo hiyo itatolewa bure kwa kila mmoja na kinachosubiriwa ni kuidhinishwa kwa usalama, kabla ya kampeni ya kuhamasisha watu kwenda kupata chanjo hiyo kuanza hivi karibuni.

Ufaransa imeagiza dozi Milioni 200 kutoka kwa kampuni mbalimbali zinazotengeneza chanjo ya Corona.

Kufikia sasa Ufaransa ina maambukizi zaidi ya Milioni Mbili.

Haya yanajri wahati Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameonya kuwa dunia huenda ikaendelea kupambana na janga la Corona kwa muda mrefu sana licha ya kuwepo kwa habari njema ya matumaini ya kupatikana kwa chanjo ambazo zipo katika mchakato wa kuthibitishwa iwapo zipo salama.

Janga la Corona limesababisha vifo vya watu Milioni Moja na Laki Tano kote duniani na wengine Milioni 65 wameambukizwa.