UJERUMANI-COVID 19-AFYA

Idadi ya vifo nchini Ujerumani yapindukia zaidi ya 19,000

Maabara ya kupima maambukizi ya virusi vya Corona nchini Ujerumani
Maabara ya kupima maambukizi ya virusi vya Corona nchini Ujerumani Marijan Murat / dpa / AFP

Idadi ya visa vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi vya Corona nchini Ujerumani imepanda hadi 1,197,709, baada ya visa 14,054 kuripotiwa siku moja iliyopita, kulingana na takwimu zilitolewa leo Jumanne na kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa cha Robert Koch (RKI).

Matangazo ya kibiashara

Taasisi hiyo pia imeripoti vifo vipya 423, na kufanya jumla ya vifo kufikia 19,342 tangu kuzuka kwa janga hilo nchini Ujerumani.

Hayo yanajiri wakati Uingereza hii leo Jumanne imeanza matumizi ya chanjo ya Pfizer / BioNTech kwa watu walio katika mazingira magumu zaidi, na kuwa nchi ya kwanza ya Magharibi kutoa mpango mkubwa wa chanjo dhidi ya virusi vya Corona, vyombo vya habari vya Uingereza vimeripoti.

Ujerumani ni mojawapo ya nchi za Ulaya ambazo zimeendelea kurekodi idadi kubwa ya visa vipya vya maambukizi.

Mlipuko wa virusi vya corona unaosababisha ugonjwa wa COVID-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa COVID-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.