MISRI-UFARANSA-DIPLOMASIA

Ziara ya Al-Sisi: Ufaransa yaitaka Misri kuheshimu haki za binadamu

Rais wa Misri  Abdel Fattah al-Sisi
Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi ©REUTERS/Mohamed Abd El Ghany

Rais Ufaransa Emmanuel Macron amesema amezungumza kwa uwazi na mwezanke wa Misri President Abdel Fattah al-Sisi kuhusu masuala ya haki za binadamu katika taifa hilo la Afrika Kaskazini huku wanaharakati wakiendelea kumshinikiza kiongozi wa Misri kuwaachilia huru wanaharakati wa kisiasa.

Matangazo ya kibiashara

Macron bila kueleza kwa kina kile alichomwambia rais Sisi, ameyasema hayo katika mkutano na wanahabari jijini Paris, baada ya kumpokea rais Sisi ambaye yupo ziarani nchini humo kwa siku mbili katika ziara inayolenga kuimarsha uhusiano kati ya nchi hiyo mbili lakini pia hali ya usalama na utulivu nchini Libya.

"Hatukubaliani kuhusu haki za binadamu," Emmanuel Macron amekiri katika mkutano na waandishi wa habari kufuatia mazungumzo na mwenzake wa Misri Abdel Fatah al-Sisi. Lakini uungwaji mkono wa Ufaransa kwa Misri hautokwenda sambamba na "masharti juu ya tofauti hiyo", kwani itakuwa haina tija na haitokuwa muhimu kwa kuzingatia ushirikiano wa nchi hizi mbili kwa mara moja, rais wa Ufaransa ameongeza.

Wakati mashirika mbalimbali ya haki za binadamu yameendelea kulaani ukandamizaji na ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Misri, rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi amedai kwamba nchi yake haipaswi kushtumiwa kama serikali ya kiimla. Kwa kutaka kujisafisha na tuhuma za ukiukwaji wa haki za binadamu, ametaja vita dhidi ya ugaidi, akibaini kwamba ni jukumu lake kuwalinda Wamisri milioni mia moja.

Viongozi hao wawili pia wamesisitiza juu ya ushirikiano wao "wa kimkakati na muhimu", kulingana na kauli ya Emmanuel Macron: Paris na Cairo wameshikamana bega kwa bega dhidi ya mgogoro wa Libya - nchi jirani ya Misri -, Paris na Cairo wanafanya kazi pamoja katika Mashariki mwa Mediterania - eneo ambapo suala la visima vya gesi limezua utata. Katika maswala haya mawili yanayohusiana, Abdel Fattah al-Sissi na Emmanuel Macron wameonyesha msimamo wa pamoja dhidi ya Uturuki, ambayo wanaishutumu sera yake katika ukanda huo.

Rais al-Sisi pia amekutana na rais wa Bunge la Seneti na Baraza la Bunge la kitaifa, wakati wabunge 70 walimwandikia barua, wakimtaka awaachilie wasomi wengi na watetezi wa haki za binadamu ambao wanazuiliwa katika magereza mbalimbali nchini Misri.