UJERUMANI-COVID 19-AFYA

Covid 19: Zaidi ya visa vpya 20,000 vyathibitishwa nchini Ujerumani

Chanjo aina ya Moderna
Chanjo aina ya Moderna Photo AP / Hans Pennink

Idadi ya visa vilivzothibitishwa vya maambukizi ya virusi vya Corona nchini Ujerumani imepanda hadi 1,218,524, baada ya visa vipya 20,815 kuripotiwa siku moja iliyopita, kulingana na takwimu zilizotolewa leo Jumatano na kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa cha Robert Koch (RKI).

Matangazo ya kibiashara

Taasisi hiyo pia imeripoti vifo vipya 590, na kufikisha jumla ya vifo 19,932 tangu kuzuka kwa janga hilo nchini Ujerumani.

Ujerumani ni mojawapo ya nchi za Ulaya ambazo zimeendelea kurekodi idadi kubwa ya visa vipya vya maambukizi.

Mlipuko wa virusi vya corona unaosababisha ugonjwa wa COVID-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa COVID-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.