UJERUMANI-COVID 19-KONGAMANO

Mkutano wa usalama wa Munich waahirishwa kwa sababu ya COVID-19

Angela Merkel wa Ujerumani
Angela Merkel wa Ujerumani Fabrizio Bensch/pool photo via AP

Mkutano wa usalama wa Munich ambao unawaleta pamoja viongozi mbalimbali wa ulinzi na usalama katika mji mkuu wa Bavaria kila mwaka mnamo Februari utahirishwa kwa sababu ya janga la Corona, waandaaji wa mkutano huo wamesema leo Jumatano.

Matangazo ya kibiashara

Mwenyekiti wa mkutano huo Wolfgang Ischinger amesema anaafuta tarehe mpya ya mkutano huo ambao pia unajulikana kama "Defense of Davos".

"Lengo langu ni kuweza kuandaa Mkutano wa usalama wa Munich mwaka 2021 katika muundo wa jadi pamoja na vikao ambavyo wahusika watashiriki moja kwa moja bila kupitia njia za video, ikiwa hali inaruhusu," ameongeza.

Mkutano wa Usalama wa Munich ni tukio la kila mwaka linalowakutanisha watalaamu wa usalama na wanasiasa, viongozi wa kijeshi na sekta ya ulinzi kutoka duniani kote.

Katika kipindi cha miongo kadhaa iliopita, mkutano wa usalama wa Munich umekuwa mkusanyiko muhimu wa jumuiya ya kimkakati ya kimataifa. Mkutano huo unanuwia kukuza dhana ya utatatuzi wa amani wa migogoro na ushirikiano wa kimataifa na una lengo makhsusi la kuimarisha ushirikiano wa mataifa ya kanda ya Atlantiki.

Mkutano huo uliasisiwa na kuendeshwa hadi leo hii, na mwanadiplomasia wa zamani wa Ujerumani Wolfgang Ischinger. Ukurasa huu ni mkusanyiko wa karibuni wa maudhui za DW kuhusu mkutano huo wa kila mwaka wa Munich.