UJERUMANI-COVID 19-AFYA

Merkel kujadili na Länder kuhusu kuongezwa kwa vizuizi dhidi ya Corona nchini Ujerumani

Kansela wa Ujerumani  Angela Merkel
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel Fabrizio Bensch/pool photo via AP

Kansela Angela Merkel atajadili na viongozi wa majimbo (Länder) siku ya Jumapilikuhusu kuimarishwa kwa hatua za raia kutotembea nchini Ujerumani wakati idadi ya maambukizi mapya inaendelea kuongezeka kila kukicha, vyanzo rasmi vimebaini kulingana na shirika la habari la REUTERS.

Matangazo ya kibiashara

Ujerumani imekuwa katika "hatua nyepesi" kwa wiki sita. Baa na mikahawa vimefungwa, lakini biashara na shule vimebaki wazi. Mikoa mingine tayari imeamua kuongeza vikwazo dhidi ya Corona.

Mazungumzo ya Jumapili yatahusu kufungwa kwa maduka kabla ya likizo ya Krismasi, hivyo vyanzo vimeongeza.

Waziri wa Uchumi Peter Altmaier ameyaambia magazeti ya majimbo ya shirika la habari la RND kwamba wodi za wagonjwa mahututi katika hospitali za Ujerumani ziinakaribia kujaa na mamlaka hazingeweza kuruhusu Krismasi ipite kabla ya kuchukua hatua.

Hayo yanajiri wakati Idadi ya visa vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi vya Corona imepanda hadi 1,300,516, baada ya visa 28,438 kuripotiwa siku moja iliyopita, kulingana na takwimu zilizotolewa leo Jumamosi na kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa cha Robert Koch (RKI).

Taasisi hiyo pia imeripoti vifo vipya 496, na kusababisha jumla ya vifo 21,466 tangu kuzuka kwa janga hilo nchini Ujerumani.