COVID 19-ITALIA

COVID 19: Karibu kesi mpya 20,000 zathibitishwa nchini Italia

Vipimo vya Corona
Vipimo vya Corona REUTERS/Kacper Pempel

Wizara ya Afya ya Italia imebaini kwamba visa vipya 19,903 vya maambukizi ya virusi vya Corona vimeripotiwa nchini humo na vifo vipya 649 vimethibitishwa katika muda wa saa 24 zilizopita.

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Ijumaa Italia ilirekodi visa 18,727 vya maambukizi na vifo 761.

Jumla ya watu 64,036 wamefariki dunia kutokana na ugonjwa huo nchini Italia, ambayo ilikuwa nchi ya kwanza ya magharibi kuathirika na COVID-19.

Idadi ya wagonjwa wa COVID-19 katika hospitali nchini humo ilifikia 28,066 Jumamosi na 3,199 wako chini ya uangalizi mkubwa.