UHOLANZI-CORONA

COVID 19: Uholanzi yakabiliwa na ongezeo la wagonjwa tangu mwezi Oktoba

Maafisa wa afya wanaopima maambukizi ya virusi vya Corona nchini Uholanzi
Maafisa wa afya wanaopima maambukizi ya virusi vya Corona nchini Uholanzi REUTERS

Uholanzi imerekodi zaidi ya visa 9,000 vya maambukizi ya virusi vya Corona katika muda wa saa 24 zilizopita, kiwango ambacho hakijafikiwa tangu Oktoba, zimebaini takwimu zilizotolewa Jumamosi na maafisa wa afya.

Matangazo ya kibiashara

Baraza la mawaziri linatarajiakukutana leo Jumapili kujadili uwezekano wa kuchukua hatua kali kuhusiana na raia kutembea na shughuli mbalimbali kabla ya sikukuu ya Krismasi.

Idadi ya visa vya maambukizi nchini Uholanzi sasa inazidi 600,000 na 10,000 wamefariki dunia.

Mlipuko wa virusi vya corona unaosababisha ugonjwa wa COVID-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa COVID-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.