EU

Chanjo ya COVID-19: Mamlaka ya dawa Ulaya yakabiliwa na shinikizo

Bendera za umoja wa Ulaya
Bendera za umoja wa Ulaya AFP

Wakati kampeni za chanjo zimeanza katika nchi kadhaa duniani, Mamlaka ya dawa barani Ulaya imejikuta inakabiliwana shinikizo kutoka nchi za Ulaya, wakiwa na nia ya kuanza ya kwao.

Matangazo ya kibiashara

Marekani, Canada, Singapore, Bahrain na hata Uingereza wameanza kampeni yao ya chanjo dhidi ya COVID-19 wakati nchi kadhaa za Umoja wa Ulaya, zikitia zikiongeza hatua za kukabiliana na janga hilo kwa hofu ya kuongezeka kwa maambukizi zaidi wakati zikikaribia sikukuu za mwisho wa mwaka tena ongeza uchafuzi.

Chini ya shinikizo kutoka kwa nchi kadhaa za Ulaya, ikiongozwa na Ujerumani, Mamlaka ya dawa Ulaya imekubali kutathimini chanjo ya Pfizer-BioNTech mnamo Desemba 21, wiki moja kabla kuliko ilivyotarajiwa.

Mamlaka ya dawa Ulaya, AEM, imebaini kwamba ilipokea Jumatatu "takwimu mpya" kutoka maambara ya Pfizer-BioNTech zilizoombwa na kamati ya mamlaka hiyo inayohusika na kukagua dawa kwa matumizi ya binadamu "na kwamba" mkutano wa dharura (wa kamati hiyo) umepangwa kufanyika Desemba 21 ili kuamua ". Kuhusu chanjo ya Moderna, tarehe iliyopangwa ni Januari 12, kama ilivyotangazwa hapo awali.

Mamlaka ya dawa Ulaya imeongeza kuwa itaamua tu "ikiwa takwimu juu ya ubora, usalama na ufanisi wa chanjo hiyo ni thabiti na imekamilika kubaini ikiwa manufaa y chanjo hiyo iko juu ya hatari zake.

Shinikizo kutoka nchi za Ulaya

Kwa siku kadhaa, nchi tofauti za Ulaya zimekuwa zikishinikiza Mamlaka ya dawa Ulaya kupata idhini ya kuzindua kampeni yao ya chanjo. "Lengo ni kupata idhini kabla ya Krismasi," Waziri wa Afya wa Ujerumani Jens Spahn alisema Jumanne wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Berlin. "Tunataka kuanza chanjo nchini Ujerumani kabla ya mwisho wa mwaka," aliongeza.

Wakatu huo huo Waziri wa Afya wa Italia alisema kuwa ana matumaini AEM "itaweza kutoa idhini yake kwa chanjo ya Pfizer-BioNTech mapema kuliko ilivyotarajiwa."