UTURUKI-URUSI

Mevlut Cavusoglu: Uturuki haitaacha kutumia makombora ya Urusi

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan
Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan Presidential Press Office/Handout via REUTERS

Serikali ya Uturuki haitarudi nyuma kwa kununua mfumo wa ulinzi wa makombora ya S-400 kutoka Urusi na itachukua hatua za kulipiza kisasi baada ya kutathmini vikwazo vya Marekani vilivyowekwa kutokana na ununuzi huo, waziri wa mambo ya nje ameahidi Alhamisi

Matangazo ya kibiashara

Vikwazo hivi vibaya kisheria na kisiasa vinakiuka haki za kujitawala za Uturuki na hazitaathiri Ankara, ameongeza Mevlut Cavusoglu katika mahojiano na kituo cha Kanal 24.

Jumatatu Marekani iliweka vikwazo dhidi ya sekta ya ulinzi ya Uturuki (SSB), rais wake na wafanyakazi watatu kutokana na kununua mfumo wa ulinzi wa makombora ya S-400 kutoka Urusi, ambayo Washington ilisema hauendani na mfumo wa NATO, ambapo Uturuki mwanachama wake.

Siku ya Jumatano rais Recep Tayyip Erdogan aliikosoa hatua ya Marekani ya kuiwekea vikwazo nchi hiyo, akisema ilikuwa ni shambulizi dhidi ya haki ya uhuru wa taifa hilo na iliyonuia kuidhoofisha sekta ya ulinzi na kusema haitafanikiwa.

Erdogan alitoa matamshi hayo kwa mara ya kwanza tangu Marekani ilipoiwekea vikwazo mapema wiki hii, na kuahidi kuzikabili changamoto zitakazotokana na vikwazo hivyo.