URUSI

Urusi yatupilia mbali madai ya sumu dhidi ya Nalvany

Alexei Navalny  mwanasiasa wa upinzani nchini Urusi
Alexei Navalny mwanasiasa wa upinzani nchini Urusi AP Photo/Pavel Golovkin

Urusi imefutilia mbali ripoti ya mwisho ya uchunguzi wa uandishi wa habari ulioihusisha timu ya FSB, idara ya usalama ya Urusi, kwa kumpa sumu kiongozi wa upinzani na mkosaji mkuu wa Putin, Alexeï Navalny.

Matangazo ya kibiashara

Urusi imeitaja ripoti hiyo kuwa ni ya 'kichekesho'.

"Tumeizoea Marekani na nchi zingine za Magharibi kuituhumu Urusi kwenye vyombo vya habari, hususan madai ya uhalifu wa kimtandao na madai ya Navalny kupewa sumu mara mbili au hata mara tatu.

" Waziri wa Mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov amesema katika mkutano na waandishi wa habari huko Zagreb akiwa pamoja na mwenzake wa Kroatia Gordan Grlic Radman kwa kutumia vyanzo mbalimbali vya takwimu, hususan data za  ndege na simu za kiganjani, tovuti ya Bellingcat na kituo cha cha habari cha Urusi cha The Insider, Jumatatu walichapisha matokeo ya uchunguzi wa pamoja   uliofanywa kwa ushirikiano na vituo vya habari vya Der Spiegel na CNN.

Wamewataja watu binafsi na maabara na wanadai kwamba maafisa wa F SB,iliyochukuwa nafasi ya KGB, "iliyobobea katika silaha za kemikali, kemia na dawa" walimfuatilia kwa siri Alexei Navalny zaidi ya mara 37 katika miaka minne iliyopita wakati wa safari zake nchini kote Urusi.

Akijibu kuhusu uchunguzi huo, Alexei Navalny alisema siku ya Jumatatu kwamba ukweli sasa umethibitishwa kuhusua sumu aliyopewa.

Mamlaka ya Urusi imekuwa ikikanusha madai ya kumuua Alexeï Navalny, mmoja wa wapinzani wakuu wa Rais Vladimir Putin, ambaye aliyepoteza fahamu mwezi Agosti akiwa katika ndege iliyokuwa ikitoka Siberia kwenda Moscow.

Siku mbili baada ya hali yake kuzidi kudhoofika, Alexeï Navalny alisafirishwa nchini Ujerumani, ambako anaishi kufikia sasa baada ya kutibiwa kwa karibu mwezi mmoja katika hospitali ya Charité huko Berlin.