UJERUMANI

Corona: Karibu visa vipya 34,000 vyathibitishwa nchini Ujerumani

Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel
Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel REUTERS/Annegret Hilse/File Photo

Idadi yavisa vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi vya Corona nchini Ujerumani imepanda hadi 1,439,938, baada ya visa vipya 33,777 kuthibitishwa siku moja iliyopita, kulingana na takwimu zilizotolewa leo Ijumaa na kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa cha Robert Koch (RKI).

Matangazo ya kibiashara

Taasisi hiyo pia imeripoti vifo vipya 813, na kufikisha jumla ya vifo 24,938 tangu kuzuka kwa janga hilo nchini Ujerumani.

 

Mlipuko wa virusi vya Corona unaosababisha ugonjwa wa COVID-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa COVID-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.