IRAN-UN

Nyuklia: Iran yafutilia mbali pendekezo wa IAEA juu uwezekano wa mkataba mpya

Mitambo ya kurutubisha Urani nchini Iran.
Mitambo ya kurutubisha Urani nchini Iran. 网络。

Iran imetupilia mbali pendekezo la mkurugenzi mkuu wa shirika la kimataifa la kudhibiti nishati ya nyuklia (IAEA) ambaye anaona ni muhimu kujadili mkataba mpya kuhusu mpango wake wa nyuklia mara tu utawala wa Joe Biden utakapochukuwa hatamu ya uongozi.

Matangazo ya kibiashara

"Kuwasilisha tathmini ya jinsi ahadi (zilizounganishwa na makubaliano ya 2015) inavyotekelezwa inakwenda mbali kabisa na mamlaka ya  shirika la kimataifa la kudhibiti nishati ya nyuklia na inapaswa kuepukwa," balozi wa Iran kwenye shirika la IAEA, Kazem Gharibabadi ameandika kwenye ukurasa wake aw Twitter.

 

Siku ya alhamisi katika mahojiano na shirika la habari la REUTERS, Rafael Grossi, mkurugenzi mkuu wa IAEA, alisema kwamba kufufuliwa kwa mfumo wa mpango wa nyuklia wa Iran kutokana na kuchaguliwa kwa Joe Biden kutahitaji mkataba mpya.

 

Hakuna hoja, ya kurudi kwa masharti ya Mpango wa Utekelezaji wa Pamoja (JCPoA) uliofikiwa mwezi Julai 2015 huko Vienna. Iran imekiuka mkataba huu mara nyingi sana," Rafael Grossi alisema.

 

Donald Trump alikashifu mkataba wa Vienna mnamo mwaka 2018,na kuamuwa kuongeza vikwazo dhidi ya Iran.

 

Joe Biden, atachukua hatamu ya uongozi wa nchi mnamo Januari 20, amebaini kwamba anatamani kubadili sera ya "shinikizo kubwa" kwa Iran inayotekelezwa na Donald Trump na kuanzisha tena mbinu nyingine ya kidiplomasia.

 

Tehran, kwa upande wake, ilisema ina uhakika kwamba Marekani itarejea kwenye mkataba wa kimataifa juu ya mpango wa nyuklia wa Jamhuri ya Kiislamu uliofikiwa mnamo mwaka2015 na kwamba vikwazo dhidi ya Iran vitaondolewa baada ya kuapishwa kwa Joe Biden.