ITALIA-COVID 19

Covid-19: Italia kuchukuwa masharti mapya wakati wa sikukuu

Waziri Mkuu wa Italia  Giuseppe Conte
Waziri Mkuu wa Italia Giuseppe Conte Yara Nardi/Reuters

Italia inajiandaa kuchukuwa masharti mapya ya kuzua watu kutembea wakati wa sikuu ya Krismasi lakini pia sikuu ya Mwaka Mpya ili kukabiliana na janga la COVID-19 ambalo linaendelea kusababisha maafa makubwa duniani.

Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huo uliotangazwa Ijumaa, Desemba 18 jioni na Waziri Mkuu wa Italia  Giuseppe Conte, ili kuzuia ongezeko la maambukizi nchini humo.

Waziri Mkuu wa Italia Giuseppe Conte alitangaza Ijumaa jioni kwamba nchi hiyo itachukua masharti mapya ya kuzuia watu kutembea kuanzia Desemba 21 hadi Januari 6, kwa sababu ya janga Corona.

Italia ilikuwa tayari imepanga kuongeza hatua za kudhibiti ugonjwa hatari wa COVID-19 na serikali  imeamua kuchukua hatu kali zaidi.

Masharti ya  kutotoka nje yataendelea kushuhudiwa nchini humo hadi mapema mwezi Januari mwaka 202.