UINGEREZA-WHO

Hofu baada ya Uingereza kugundua aina mpya ya virusi vinavyoenea kwa kasi

Hofu baada ya aina mpya ya virusi kuthibitishwa Uingereza.
Hofu baada ya aina mpya ya virusi kuthibitishwa Uingereza. NIAID-RML via AP

Shirika la afya duniani, WHO, limesema linafanya mawasiliano ya karibu na nchi ya Uingereza, kuhusiana na aina mpya ya virusi vya Corona ambavyo vimeonesha usugu.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa kutoka Uingereza zinasema kuwa aina mpya ya virusi, vinaenea kwa kasi zaidi kuliko vile vya awali, lakini hawaamini ikiwa ni hatari.

Tayari maeneo mengi ya miji ya Kusini na mashariki mwa Uingereza, kumetangazwa makataa zaidi ya watu kutembea ili kudhibiti kuenea kwa maambukizi.

Hadi sasa hakuna ushahidi kuwa virusi hivi vilivyogunduliwa vinaonesha utofauti na chanjo ambayo inatolewa.

Siku ya Jumapili, serikali ya Uholanzi ilitangaza masharti mapya kwa wasafiri kutoka Uingereza, saa chache baada ya aina mpya ya virusi kuthibitishwa, ambapo masharti haya yatasalia hadi Januari Mosi mwaka ujao.

Uamuzi wa Uholanzi umekuja baada ya uchunguzi walioufanya kubaini aina mpya ya virusi asili yake ni Uingereza.