BREXIT-UINGEREZA-EU

Mkwamo kuhusu mkataba wa Brexit hasa masuala ya uvuvi

Waziri mkuu wa Uingereza, Boris Johnson.
Waziri mkuu wa Uingereza, Boris Johnson. REUTERS/Toby Melville

Mvutano kuhusu haki za uvuvi kati ya Uingereza na Umoja wa Ulaya unatishia matokeo ya mazungumzo ambayo yanaanza tena Jumapili hii kupata makubaliano ya baada ya Brexit, siku kumi tu kabla ya pande hizo mbili ktalakiana.

Matangazo ya kibiashara

Hakutakuwa na mpango wowote isipokuwa wa "mabadiliko makubwa" katika msimamo wa Brussels katika siku zijazo, chanzo cha Uingereza kimeonya Jumamosi jioni katika taarifa kwa vyombo vya habari.

 

Duru kutoka pande zote zimesema kama hakuna upande utakaolegeza msimamo kuhusu uvuvi katika eneo la bahari la Uingereza, basi nchi hiyo itajiondoa katika soko la pamoja ifikapo usiku wa manane wa Desemba 31, bila ya mkataba wa kibiashara kati ya Umoja wa Ulaya na Uingereza.

 

Suala hilo la uvuvi ndiyo jambo pekee linalozuia kufikiwa makubaliano kabla ya Januari mosi ili kuzuia kurejeshwa kwa kanuni za ushuru kati ya Uingereza na Umoja wa Ulaya.

 

 Bunge la Umoja wa Ulaya limesema kuwa muda wa mwisho wa kupatikana mkataba unapaswa kuwa usiku wa leo Jumapili ili kuwezesha mkataba huo kuidhinishwa kabla ya mwisho wa mwaka.