COVID19-AUSTRALIA

Australia: Safari za ndege kuelekea Sydney zasitishwa

Jiji la Sydney, Australia
Jiji la Sydney, Australia ©REUTERS/Steven Saphore

Safari kadhaa za ndege zilizokuwa zimepangwa leo Jumatatu kuelekea mji mkuu wa Australia, Sydney, zimsitishwa kutokana na ongezeko la visa vingi vya maambukizi ya virusi vya Corona.

Matangazo ya kibiashara

Maafisa wa afya wameendelea kutoa ujumbe kuwaonya wakaazi wa mji huo wakati wimbi jipya la mlipuko wa coronavirus linatishia mji huo mkubwa wa Australia ssiku nne kabla ya Krismasi.

Angalau maeneo 50 kote Sydney, pamoja na mikahawa na maduka makubwa, kumeripotiwa visa vya maambukizi. Mamlaka katika mji huo zimetoa wito kwa wale ambao wametembelea maeneo haya kupimwa haraka na kujitenga.

"Safari kadhaa za ndege zitafutwa (...) Tutakuwa tukiwasiliana moja kwa moja na wateja walioambukizwa virusi vya Corona," shirika la ndege la Qantas Airways limesema.

Australia hadi sasa imefanikiwa pakubwa kudhibiti janga la COVID-19, ikilinganishwa na nchi zingine zilizoendelea, lakini kuonekana kwa hivi karibuni kwa visa vipya vya maambukizi, kumeongeza hofu ya mgogoro mkubwa wa kiafya nchini humo. Karibu visa 28,200 vya maambukizi ya virusi vya Coronana vifo 908 vimerekodiwa nchini.