EU

Coronavirus: Nchi za Ulaya zasitisha safari za ndege na Uingereza

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson katika mbele ya Baraza la Wawakilishi huko London, Oktoba 21, 2020.
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson katika mbele ya Baraza la Wawakilishi huko London, Oktoba 21, 2020. AFP

Mataifa ya bara Ulaya yameanza kuweka vikwazo vya safari za ndege kati yao na Uingereza, baada ya taifa hilo kushuhudia ongezeko kubwa la maambukizi ya COVID-19.

Matangazo ya kibiashara

Mataifa ya bara Ulaya ambayo yametangaza kusitisha safari kati ya nchi zao na Uingereza ni pamoja na Ufaransa, Ujerumani, Italia, Ubelgiji na Ireland.

Baadaye leo, viongozi wa Umoja wa Ulaya watakutana kuweka mikakati ya pamoja ya kukabiliana na mlipuko huu mpya hasa nchini Uingereza.

Jiji la London na maeneo ya Kusini Mashariki mwa taifa hilo, ndiyo yanayoshuhudia ongezeko kubwa la mamabukizi hayo, licha ya serikali nchini humo kutangaza mikakati mipya ya kuzuia mamabukizi zaidi kuelekea sikukuu ya Krismasi siku ya Ijumaa.

Waziri wa Afya nchini Uingereza Matt Hancock amesema maambukizi haya mapya yanaonekana kuwa magumu kuyadhibti, baada ya watu Elfu 13 kuambukizwa siku ya Jumapili.

Ongezeko hili limekua, licha ya Uingereza kuwa nchi ya kwanza duniani kuanza kutumia chanjo ya kuzuia maambukizi ya COVID-19 ambayo yamesababisha vifo vya watu zaidi ya Elfu 67, huku wengine zaidi ya Milioni wakiambukizwa.