UJERUMANI

Coronavirus: Zaidi ya visa vipya 19,500 vyathibitishwa nchini Ujerumani

Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel
Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel 路透社

Idadi ya visa vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi vya Corona nchini Ujerumani imepanda hadi 1,530,180, baada ya visa vipya 19,528 kuripotiwa siku moja iliyopita, kulingana na takwimu zilizotolewa leoJumanne na kituo cha kuzuia na kudhibiti magonjwa cha Robert Koch (RKI).

Matangazo ya kibiashara

Kituo hiki pia kimeripoti vifo vpiya 731, na kufikisha jumla ya vifo 27,006 tangu kuazuka kwa janga hilo nchini Ujerumani.

Wakati huo huo Marekani imevuka kizingiti cha visa milioni 18 vilivyorekodiwa vya virusi vya Corona Jumatatu wiki hii, na zaidi ya vifo 319,000 tangu kuzuka kwa janga hilo nchini humo, kulingana na kituo kinachozuia na kudhibiti magonjwa cha Johns Hopkins.

Mlipuko wa virusi vya Corona unaosababisha ugonjwa wa COVID-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa COVID-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.