UINGEREZA

Brexit: London na Brussels wana imani ya kufikia mkataba

Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya kwenye mazungumzo hayo  Michel Barnier na Mwakilishi wa Waziri Mkuu wa Uingereza   David Frost wakiwa jijini Brussels
Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya kwenye mazungumzo hayo Michel Barnier na Mwakilishi wa Waziri Mkuu wa Uingereza David Frost wakiwa jijini Brussels Oliver Hoslet/Pool via REUTERS

Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen anatarajia kukutana na Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson leo Alhamisi  baada ya usiku wa mwisho wa mazungumzo kuhusu mkataba wa baada ya Uingereza kujitoa katiak umoja wa Ulaya (Brexit). 

Matangazo ya kibiashara

Pande hizo mbili zina matumaini  ya kufikia maelewano ya kihistoria siku moja kabla ya Krismasi.

Mazungumzo haya yamepangwa kufanyika leo Alhamisi "ikiwa mambo yatakwenda sawa". Mazungumzo hayo yanaweza kufuatiwa na taarifa kwa waandishi wa habari, kilisema chanzo cha Umoja wa Ulaya.

Matokeo katika mkesha wa Krismasi wa mazungumzo haya ya mazuri, ambayo yalianza mwezi Machi, yatawezesha pande hizo mbili kujiepusha na "kujitoa ya bila mkataba" ambapo ni aibu katika ngazi ya kisiasa na  ni hatari katika kiwango cha uchumi.

Chanzo kutoka Umoja wa Ulaya kilibaini siku ya Jumatano kwamba kuna "uwezekano kubwa" wa kufikia mkataba. Lakini "mazungumzo hayajamaliika," kimeonya chanzo hicho hicho leo Alhamisi asubuhi.

Kulingana na chanzo cha serikali ya Ufaransa, Waingereza wameonyesha utashi wa kutoha na kupiga "hatua kubwa", hasa kuhusu suala la uvuvi, kikwazo cha mwisho katika mazungumzo hayo.