UFARANSA

Coronavirus: Kampeni ya chanjo kuanza Ufaransa

Maeneo ya jiji la Paris likiwa halina watu kutokana na makata ya watu kutembea.
Maeneo ya jiji la Paris likiwa halina watu kutokana na makata ya watu kutembea. Reuters

Zoezi la kutoa chanjo dhidi ya virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa hatari wa COVID-19 linatarajia kuanza leo Jumapili nchini Ufaransa.

Matangazo ya kibiashara

Wazee ishirini na wahudumu wa afya watakuwa wa kwanza kupewa chanjo dhidi ya COVID-19 leo Jumapili, siku chache kabla ya mwaka 2020 kumalizika, mwaka ambao ulishuhudia vifo 62,500 nchini Ufaransa kutokana na Corona.

Licha ya kuzinduliwa kwa kampeni hii ya chanjo, Olivier Véran, Waziri wa Afya, amesema kuna uwezekano wa marufu ya kutotembea ichukuliwe kwa mara ya tatu ikiwa hali itaendelea kuwa mbaya zaidi.

Nchi nyingi za Umoja wa Ulaya zilianza rasmi zoezi hilo jana Jumamosi, wakati aina mpya kirusi kinachosambaa kwa kasi kikiripotiwa katika mataifa ya Ulaya.

Aina hii ya kirusi kipya kinachosambaa kwa kasi kilichoanzia nchini Uingereza imegunduliwa nchini Canada, Sweden, Ufaransa, Uhispania na Japan.